WANANCHI 15 WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUTO KUWA NA VYOO.

LONGIDO,ARUSHA : Wananchi 15 wa kijiji cha Gebailumbwa wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya kwa Makosa Matatu ikiwemo kutokuwa na Vyoo na hivyo kusababisha Magonjwa Ya Mlipuko.
-
Makosa yao ni , Mnamo mwaka 2016 na April mwaka huu watuhumiwa wote walikahidi Amri halali ya kuchimba Vyoo Jambo ambalo ni Kinyume na Sheria ya Afya ya mwaka 2009.
Lingine ni kukataa kujenga Vyoo ili kuepuka Magonjwa ya Mlipuko kama walivyo elekezwa na Afisa Afya.
-
Washitakiwa hao walishindwa kukidhi Masharti ya Dhamana na kurudishwa katika Gereza la Kisogo hadi Mei 16 kesi yao itakapo tajwa tena.

1 comment:

Powered by Blogger.