Chanzo cha Maji kutoka Ziwa Victoria Kina Uwezo wa Kusambaza Maji Mikoa 3

Chanzo hiki cha maji kutoka Ziwa Victoria kilijengwa eneo la Ihelele wilayani Misungwi.

Kuna mitambo miwili ya kusukuma maji (umewashwa mtambo mmoja tu) na unasukuma maji kwenda kwenye tenki lenye ukubwa wa zaidi ya mita 300.

Wanufaika kwa sasa ni wananchi wa mkoa wa Shinyanga na baadae Tabora na hata Singida na Dodoma. Wilaya ya Misungwi imeanza kujenga miundombinu ya maji ikiwemo maboma na manteki ili nayo inufaike na maji haya ambayo ni safi na salama.

Naambiwa mashine zilizopo hapa zinapaswa kuwaka angalau miezi mitatu bila kuzimwa lakini kutokana na matumizi ya maji kwa sasa kuwa kidogo, inalazimika kuzimwa maana tenki huwa linajaa (kasi ya maji kuingia ni kubwa kuliko matumizi na hapo inatumika mashine moja).

Kaimu Mkuu wa kituo hiki, Cheyo Kanuda anasem ikiwa miundombinu ya maji itaimarishwa, basi chanzo hiki  cha maji KASHWASA kina uwezo wa kusambaza maji mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Tabora, Singida na Dodoma.

COMMENT                      SHARE

1 comment:

Powered by Blogger.